CORRECT LYRICS

Lyrics : Kwaru

Mmmh aaah aah, mmmh aaah
Aaaah, aah

Roho ingekuwa na macho ungejionea
Moyo haufanyi kificho ukiotea
Mimi kifigiso nacho ungeongea
Mwili wangu rojorojo nanyong'onyea

Chungu nilichopika wamepakua wenzangu
Huruma napokutishwa wamechukua wezangu

Na kitabu chetu cha mapenzi, kurasa wamechanachana
Hazisomeki tena tenzi, vimepoteza maana

Mpofu moyo wangu, ulishindwa ona
Hukuandikwa wa kwangu limenikaba nalitema

Kwaru kwa kwaru kwaru
Kachukua kisu ye anaukwarua
Kwaru kwa kwaru kwaru
Moyo wangu unaumia
Kwaru kwa kwaru kwaru
Ye kwa nguvu anaukwarua
Kwaru kwa kwaru kwaru
Jamani moyo wangu unaumia

Eh langu tatizo
Nachuna najimaliza
Mi nakesha kumwaza
Naweweseka lake jina, ooh jina
Oh basi kwa unyonge najikaza niache kulia
Maana kwake bahati sina, ooh sina
Maumivu ameipora furaha yangu
Oooh amekwenda nayo
Na zangu mbivu zimeniozea
Hasara kwangu, oooh yatapita hayo

Mpofu moyo wangu, ulishindwa ona
Hukuandikwa wa kwangu limenikaba nalitema


Kwaru kwa kwaru kwaru
Kachukua kisu ye anaukwarua
Kwaru kwa kwaru kwaru
Moyo wangu unaumia
Kwaru kwa kwaru kwaru
Ye kwa nguvu anaukwarua
Kwaru kwa kwaru kwaru
Jamani moyo wangu unaumia