CORRECT LYRICS

Lyrics : Napambana

Naamka asubuhi, sina hata buku shi ndala
Cha kukila sijui, bora hata pa kulala
Chumbani matandabui, mende wamefanya utawala
Na mjomba panya haelewi, riziki yake hasara

Eh kwachakwacha, nakwenda nakwenda
Sijakubali kudoda hii ngoma haisambii
Na ndoto za alinacha, sijapenda sijapenda
Aliekupa kigoda, mi atanipa kumbi

Eh nipate ntoke patupu (kawaida iyo)
Siku nzima niambulie buku (ndo yakwangu sijaiba iyo)
Usiniulize naishije mjini (napambana)
Niokote machupa niuze siso (napambana)
Hata nkidanga jama niacheni (napambana)
Niwe kondakta ubungo migomigo (napambana)
Haaa, eeeh, iiih (napambana)
Aaah, eeeh, oooh (napambana)

Mama Mkubwa Lemukuu
Khadija Kopa
Boss Dela Boss
Mama Dangote

Majiamdimu majiamdimu
Saga saga saga saga

Eh, eh Mungu wangu baba baba baba
Ziitikie dua zetu waja
Tupate magari sita nane saba
Tuvae gucci fendy na miprada
Wewe acha kumbwela
Mungu habagui anawapa hadi ngedere (wewe)
Wewe (hela) tafuta hela (mchawi helaa)
Wanaokudharau watakuheshimu mbele

Eh nipate ntoke patupu (kawaida iyo)
Eti siku nzima niambulie buku (ndo yakwangu sijaiba iyo)
Usiniulize naishije mjini (napambana)
Niokote machupa niuze siso (napambana)
Hata nkidanga jama niacheni (napambana)
Niwe kondakta ubungo migomigo (napambana)
Haaa, eeeh, iiih (napambana)
Aaah, eeeh, oooh (napambana)

Mikono juu, mikono juu, mikono juu
Wapambanaji mikono juu, mikono juu, mikono juu

Asa usimcheke aloshindia chungwa
(Alie kula Kalaa)
We wa biriani shibe ileile
(Alie kula Kalaa)
Maharage robo ugali kilo kumi
(Alie kula Kalaa)
Eti kula piza baga shibe ileile
(Alie kula Kalaa)
Mama aliekula kala
(Alie kula Kalaa)
Aah, aliekula kalaa ah
(Alie kula Kalaa)